< Wimbo wa Sulemani 8 >

1 Ninatamani ungekua kama kaka yangu, aliye nyonya ziwa la mama yangu. Ili kwamba kila ningekuona nje ningekubusu pasipo mtu kunidharau. 2 Nitakuongoza na kukuleta kwenye nyumba ya mama yangu, na utanifundisha. Nitakupa mvinyo ulio chachwa unywe na baadhi ya jwisi ya komamanga. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe 3 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akiongea na wanawake wengine 4 Ninataka muape, mabinti wa wanaume wa Yerusalemu, kuwa hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Wanawake wa Yerusalemu wakizungumza 5 Ni nani huyu anaye kuja kutoka nyikani, amemuegemea mpenzi wake? Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake nimekuamsha chini ya mti wa mpera; pale mama yako alichukua mimba; pale alikuzaa, alijifungua wewe. 6 Nieka kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako, kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti. Mapenzi mazito hayana kurudi kama kwenda kuzimu; miale yake yalipuka; ni miale ya moto inayo waka, miale yenye joto kuliko moto wowote. (Sheol h7585) 7 Maji yalio zuka hayawezi kuzimisha upendo, wala mafuriko hayawezi kuondoa. Mwanaume akitoa mali zake zote kwa ajili ya upendo, ukarimu wake utadharauliwa. Kaka zake mwanamke mdogo wakizungumza wenyewe 8 Tuna dada mdogo, na matiti yake bado hayajakua. Nini tutamfanyia dada yetu siku hatakayo ahidiwa kuolewa? 9 Kama ni ukuta, tutamjengea juu yake mnara wa fedha. Kama ni mlango, tutampamba kwa mbao za mierezi. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake 10 Nilikuwa ukuta, lakini matiti yangu sasa ni kama nguzo imara; hivyo nimekomaa machoni pake. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe 11 Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baali Hamoni. Aliwakodishia wao ambao watalitunza. Kila mmoja alipaswa kuleta shekeli elfu moja za fedha kwa matunda yake. 12 Shamba langu ka mzabibu ni langu, shekeli elfu moja ni za kwako, Sulemani mpenzi, na shekeli mia mbili ni za wale wanao tunza matunda yake. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye. 13 Wewe unaye ishi katika bustani, marafiki zangu wanasikiliza sauti yako; acha na mimi niweanaye isikia pia. Mwanamke mdogo akiongea na mpenzi wake 14 Harakisha, mpenzi wangu, na uwe kama paa au mtoto wa paa kwenye milima ya manukato.

< Wimbo wa Sulemani 8 >