< Ruth 4 >

1 Ndipo Boazi akaenda kwenye lango la Bethelehemu na kukaa chini. Muda mfupi tu akaja ndugu wa karibu ambaye Boazi alimuongelea. Boazi akamwambia, “Rafiki yangu, njoo hapa na uketi. Kisha mtu huyo akaja na kuketi. 2 Ndipo Boazi akakusanya viongozi kumi wa mji na kusema, “Katini hapa.” Hivyo wakaketi. 3 Boazi alimwambia yule jamaa wa karibu, “Naomi aliyerudi kutoka mji wa Moabu, anauza sehemu ya aridhi ambayo ilikuwa ni miliki ya kaka yetu Elimeleki. 4 Nilifikiria kukujulisha na kukwambia, 'Inunue mbele ya hawa waliokaa hapa, na mbele ya viongozi wa watu wangu.' Ikiwa utapenda kuikomboa, ikomboe. Lakini ikiwa hauhitaji kuikomboa, uniambie, ili nijue, kwa kuwa hakuna mwingine wa kuikomboa isipokuwa wewe, na mimi ni mdogo wako.” Ndipo huyo mtu mwingine akasema, “Nitalikomboa.” 5 Kisha Boazi akasema, “Ile siku utakayonunua shamba kutoka mkononi mwa Naomi, yakupasa pia kumchukua Ruth Mmoabu, mjane wa mtoto wa Elimeleki, ili kuliinua jina la marehemu kama urithi wake.” 6 Ndipo yule jamaa wa karibu akasema, “Mimi siwezi kuikomboa ardhi kwa ajili yangu bila kuleta athari kwenye urithi wangu binafsi. Nakupa wewe haki ya kuikomboa kwa ajili yako mwenyewe, kwa kuwa mimi sitoweza.” 7 Hii ilikuwa ni desturi ya zamani ya Israeli kuhusu ukombozi na kubadilishana mazuri. Kudhibitisha mambo haya yote, mtu huyu alivua kiatu chake na kumpatia jirani yake; hii ilikuwa ni namna ya kufanya makubaliano ya kisheria katika Israeli. 8 Kwa hiyo huyu jamaa wa karibu akamwambia Boazi, “Inunue mwenyewe.” Kisha akavua kiatu chake. 9 Ndipo Boazi akawaambia viongozi na watu wote, “Ninyi ni mashaidi kuwa nimenunua kila kilichokuwa cha Elimeleki na kila kilichokuwa na Kileoni na Mahilon kutoka kwenye mikono ya Naomi. 10 Zaidi ya hayo kumhusu Ruth Mmoabu, mke wa Mahlon: nimempa kibali cha kuwa mke wangu, ili kuendeleza jina na urithi wa marehumu, ili kwamba jina lake lisipotee kati ya ndugu zake na lango la watu wake. Ninyi ni mashahidi leo.” 11 Watu wote na viongozi waliokuwa katika lango, walisema, “Tu mashahidi. Yahweh amfanye mwanamke huyu ambaye amekuja nyumbani kwako kama Raheli na Leya, ambao wawili hawa wameijenga nyumba ya Israeli. Na ubarikiwe katika Efrata na kuwa mashuhuri katika Bethelehem. 12 Na nyumba yako kama nyumba ya Peres, ambaye Tamari alimzalia yuda, kupitia uzao ambao Yahweh atakupatia pamoja na msichana huyu.” 13 Hivyo Boazi alimchukua Ruth, na akawa mke wake. Boazi alilala naye, na Yahweh alimruhusu kupata mimba, na alizaa mtoto wa kiume. 14 Wanamke huyu akamwambia Naomi, “Yahweh abarikiwe, ambaye hajakuacha bila ndugu wa karibu, yaani mtoto huyu. Jina lake na liwe maarufu katika Israeli. 15 Na awe kwako mrutubishaji wa maisha na mwenye ruzuku uzeeni mwako, kwa kuwa mtoto wako mkwe, ambaye anakupenda, ambaye ni bora kwako kuliko watoto wa kiume saba, amemzaa. 16 Kisha naomi akamchukua mtoto, akamlaza kifuani pake, na kumhudumia. 17 Na majirani wa yule mwanamke, wakampa jina, wakisema, “Mtoto amezaliwa kwa Naomi.” Wakawita Obedi. Ambaye alikuja kuwa baba yake na Jese, ambaye alikuja kuwa baba yake na Daudi. 18 Hiki kilikuwa ni kizazi cha Peresi: Peres alimzaa Hezroni, 19 Hezroni akamzaa Ram, Ram akamzaa Aminadabu, 20 Aminadabu akamzaa Nashon, Nashon akamzaa Salmon, 21 Salmon akamzaa Boazi, Boazi akamzaa Obed, 22 Obedi akamzaa Jese, na Jese akamzaa Daudi.

< Ruth 4 >