< Ruth 3 >

1 Naomi, mama mkwe wake, alimwambia, “Mwanangu, hainilazimu kutafuta mahali pa wewe kupumzika, ili kwamba mambo yako yaende vizuri? 2 Naye Boazi, mtu ambaye umekuwa pamoja na wasichana wake wa kazi, yeye si jamaa yetu? Tazama, jioni hii atakuwa akikung'uta shairi katika sakafu ya kupuria. 3 Kwa hiyo, oga, jipake mafuta, uvae nguo zako nzuri, na ushuke kwenda kwenye sakafu ya kupuria. Lakini usijulikane kwa mtu huyu mpaka atakapo maliza kula na kunywa. 4 Na uhakikishe kuwa, atakapo lala chini, ukumbuke mahali alipo lala ili kwamba baadaye uende kwake, ufunue miguu yake, na ulale hapo. Kisha atakuambia cha kufanya.” 5 Ruth alimwambia Naomi, “Nitafanya kila kitu ulicho sema.” 6 Alishuka kwenda kwenye sakafu ya kupuria, na alifuata maelekezo aliyopewa na mama mkwe wake. 7 Boazi alipomaliza kula na kunywa na moyo wake ulikuwa na furaha, alienda kulala chini mwisho wa sehemu ya kuhifadhia nafaka. Kisha Ruth akaenda taratibu, akaaifunua miguu ya Boazi, na kulala hapo chini. 8 Panapo usiku wa manane Boazi alisituka. Akajigeuza, na hapo mwanamke alikuwa amelala katika miguu yake! 9 Akamwambia, “Wewe ni nani?” Akajibu, “Mimi ni Ruth, mtumishi wako wa kike. Nifunike shuka lako mimi mtumishi wako wa kike, kwa kuwa wewe ni jamaa wa karibu.” 10 Boazi akamwambia, “Mwanangu, Yahweh akubariki. Umeonyesha wema mwishoni kuliko mwazoni, kwa sababu hukwenda kwa wanaume vijana, awe tajiri au masikini. 11 Na sasa, mwanangu, usiogope! Nitakufanyia yote unayosema, kwa sababu mji wa watu wangu wote wanajua kuwa wewe ni mwanamke unayestahili. 12 Nikweli kuwa mimi ni jamaa wa karibu; hata hivyo, kuna jamaa wa karibu kuliko mimi. 13 Baki hapa usiku huu, na asubuhi, ikiwa atafanya jukumu lake la jamaa wa karibu, vizuri, muache afanye jukumu lake la kindugu. lakini kama hata fanya jukumu la kindugu kwako, ndipo mimi nitafanya, kama Yahweh aishivyo. Lala mpaka asubuhi.” 14 Kwa hiyo Ruth alilala kwenye miguu ya Boazi hadi asubuhi. Lakini aliamka mapema kabla ya yeyote kuweza kumtambua mtu mwingine. Kwa kuwa alikwisha mwambia, “Isijulikane kuwa mwanamke alikuja kwenye sakafu ya kupuria.” 15 Kisha Boazi akamwambia, lete mtandio wako na uushikilie.” Alipo fanya hivyo, alipima vipimo vikubwa sita vya shairi katika mtandio na kumtwisha Ruth. Kisha Boazi akaenda mjini. 16 Ruth aliporudi kwa mama mkwe wake, alisema, “Ulifanyaje, mwanangu?” Ndipo Ruth akamwambia mambo yote aliyotendewa na mtu huyo. 17 Alimwambia, “Hivi vipimo sita vya shairi ni vile alivyonipa yeye, kwa kuwa alisema, 'Usiende mikono mitupu kwa mama mkwe wako.'” 18 Kisha Naomi akasema, “Baki hapa, mwanangu, mpaka utakapojua yatakavyo kuwa, kwa kuwa Boazi hata pumzika mpaka atakapolimaliza jambo hili leo.”

< Ruth 3 >