< Warumi 12 >

1 Kwa hiyo nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, inayokubalika kwa Mungu. Hii ndiyo ibada yenu yenye maana.
所以,弟兄們,我以上帝的慈悲勸你們,將身體獻上,當作活祭,是聖潔的,是上帝所喜悅的;你們如此事奉乃是理所當然的。
2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Fanyeni hivi mpate kujua mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yakumpendeza na kamilifu. (aiōn g165)
不要效法這個世界,只要心意更新而變化,叫你們察驗何為上帝的善良、純全、可喜悅的旨意。 (aiōn g165)
3 Kwa maana nasema, kwa sababu ya neema niliyopewa, kwamba kila mtu ambaye yupo miongoni mwenu hapaswi kufikiri zaidi juu yake mwenyewe kuliko inavyompasa kufikiri. Bali, imempasa kufikiri kwa hekima, kama ambavyo Mungu amewapa kila mmoja kiasi fulani cha imani.
我憑着所賜我的恩對你們各人說:不要看自己過於所當看的;要照着上帝所分給各人信心的大小,看得合乎中道。
4 Kwa kuwa tuna viungo vingi katika mwili mmoja, lakini si viungo vyote vina kazi moja.
正如我們一個身子上有好些肢體,肢體也不都是一樣的用處。
5 Vivyo hivyo, sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo kila mmoja kwa mwenzake.
我們這許多人,在基督裏成為一身,互相聯絡作肢體,也是如此。
6 Tuna karama zilizo mbalimbali kwa kadiri ya neema mliyopewa. Ikiwa karama ya mtu ni unabii, na itendeke kwa kadiri ya imani yake.
按我們所得的恩賜,各有不同。或說預言,就當照着信心的程度說預言;
7 Ikiwa karama ya mtu ni huduma, na atumike. Ikiwa mwingine ana karama ya kufundisha, basi, afundishe.
或作執事,就當專一執事;或作教導的,就當專一教導;
8 Ikiwa karama ya mtu ni faraja, basi, afariji. Ikiwa karama ya mtu ni kutoa, afanye hivyo kwa ukarimu. Ikiwa karama ya mtu ni kuongoza, na litendeke kwa uangalifu. Ikiwa karama ya mtu ni katika kuonesha huruma, na litendeke kwa furaha.
或作勸化的,就當專一勸化;施捨的,就當誠實;治理的,就當殷勤;憐憫人的,就當甘心。
9 Pendo lisiwe na unafiki. Chukieni uovu; mshikilie yaliyo mema.
愛人不可虛假。惡,要厭惡;善,要親近。
10 Kuhusu upendo wa ndugu, pendaneni ninyi kwa ninyi. Kuhusu heshima, heshimianeni ninyi kwa ninyi.
愛弟兄,要彼此親熱;恭敬人,要彼此推讓。
11 Kuhusu bidii, msiwe walegevu. Kuhusu roho, iweni na shauku. Kuhusu Bwana, mtumikieni.
殷勤,不可懶惰;要心裏火熱,常常服事主。
12 Furahini katika ujasiri mlionao kuhusu siku zijazo. Muwe na subira katika matatizo yenu. Mdumu katika kuomba.
在指望中要喜樂;在患難中要忍耐;禱告要恆切。
13 Mshiriki katika mahitaji ya waumini. Tafuteni njia nyingi za kuonesha ukarimu.
聖徒缺乏,要幫補;客,要一味地款待。
14 Watakieni baraka wote wanaowatesa ninyi; muwabariki na wala msiwalaani.
逼迫你們的,要給他們祝福;只要祝福,不可咒詛。
15 Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia.
與喜樂的人要同樂;與哀哭的人要同哭。
16 Muwe na nia moja ninyi kwa ninyi. Msifikiri kwa kujivuna, lakini wakubalini watu wa hali ya chini. Msiwe na hekima juu ya mawazo yenu wenyewe.
要彼此同心;不要志氣高大,倒要俯就卑微的人。不要自以為聰明。
17 Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Fanyeni mambo mema machoni pa watu wote.
不要以惡報惡;眾人以為美的事要留心去做。
18 Kama inawezekana, kama ilivyowekwa kwenu, muwe na amani na watu wote.
若是能行,總要盡力與眾人和睦。
19 Wapenzi, msijilipizie kisasi wenyewe, lakini ipisheni ghadhabu ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, '' 'kisasi ni changu; Mimi nitalipa,' asema Bwana.”
親愛的弟兄,不要自己伸冤,寧可讓步,聽憑主怒;因為經上記着:「主說:『伸冤在我,我必報應。』」
20 “Lakini ikiwa adui yako ana njaa, mlishe. Akiwa na kiu, mnyweshe. Kwa maana ukifanya hivyo, utampalia makaa ya moto juu ya kichwa chake.”
所以,「你的仇敵若餓了,就給他吃,若渴了,就給他喝;因為你這樣行就是把炭火堆在他的頭上。」
21 Usishindwe na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.
你不可為惡所勝,反要以善勝惡。

< Warumi 12 >