< Zaburi 1 >

1 Amebarikiwa mtu yule asiye enenda katika ushauri wa waovu, au kusimama katika njia ya wenye dhambi, au kukaa katika kusanyiko la wenye mizaha. 2 Bali yeye huifurahia sheria ya Yahwe, na huitafakari sheria yake mchana na usiku. 3 Atakuwa kama mti uliopandwa karibu na mkondo wa maji ambao huzaa matunda yake kwa majira yake, ambao majani yake hayakauki; lolote afanyalo litafanikiwa. 4 Waovu hawako hivyo, wao badala yake ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. 5 Kwa hivyo waovu hawatasimama katika hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki. 6 Kwa kuwa Yahweh huikubali njia ya wenye haki, njia ya waovu itaangamizwa.

< Zaburi 1 >