< Zaburi 99 >

1 Yahwe anatawala; mataifa na yatetemeke. Ameketi juu ya makerubi; nchi inatetemeka. 2 Yahwe ni mkuu katika Sayuni; naye ametukuka juu ya mataifa yote. 3 Nao walisifu jina lako kuu na lenye kutisha; yeye ni mtakatifu. 4 Mfalme ana nguvu, naye hupenda haki. Wewe umeimarisha haki; umetenda haki na hukumu katika Yakobo. 5 Msifuni Yahwe Mungu wetu na sujuduni miguuni pake. Yeye ni mtakatifu. 6 Musa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, na Samweli alikuwa miongoni mwa wale walio muomba Yeye. Walimuomba Yahwe, naye akawajibu. 7 Alizungumza nao toka nguzo ya wingu. Walizishika amri zake takatifu na sheria ambazo aliwapatia. 8 Wewe uliwajibu, Yahwe Mungu wetu. Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe, lakini uliye adhibu matendo yao ya dhambi. 9 Msifuni Yahwe Mungu wetu, na mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, maana Yahwe Mungu wetu ni Mtakatifu.

< Zaburi 99 >