< Zaburi 93 >

1 Yahwe anatawala; amevikwa adhama; Yahwe amejivika na kujifunga nguvu. Ulimwengu umeimalishwa; hauwezi kusogezwa. 2 Kiti chako cha enzi kimeimarishwa nyakati za kale; umekuwepo siku zote. 3 Bahari zimeinuka, Yahwe; zimemepaza sauti zao; mawimbi ya bahari yapiga ghasia na ngurumo. 4 Zaidi ya ghasia ya mawimbi mengi, mawimbi ya bahari yenye nguvu, Yahwe aliye juu ni mwenye nguvu. 5 Amri zako makini ni za kuaminika sana; utakatifu huipamba nyumba yako, Yahwe, milele.

< Zaburi 93 >