< Zaburi 87 >

1 Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu; 2 Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo. 3 Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. (Selah) 4 Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'” 5 Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha. 6 Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” (Selah) 7 Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”

< Zaburi 87 >