< Zaburi 82 >

1 Mungu amesimama katika kusanyiko la mbinguni; katikati ya miungu anahukumu. 2 Hata lini mtahukumu bila haki na kuonesha upendeleo kwa waovu? (Selah) 3 Wateteeni maskini na yatima; dumisheni haki kwa aliyetaabishwa na fukara. 4 Muokoeni maskini na muhitaji; watoeni mkononi mwa waovu. 5 Hawajui wala hawaelewi; hutembea gizani; misingi yote ya nchi imebomoka. 6 Mimi nilisema, “Ninyi ni miungu, na ninyi nyote wana wa Mungu aliye Juu. 7 Hata hivyo mtakufa kama wanadamu na mtaanguka kama mmoja wa wakuu.” 8 Uinuke, Ee Mungu, uihukumu nchi, maana unaurithi katika mataifa yote.

< Zaburi 82 >