< Zaburi 8 >

1 Yahweh Bwana wetu, ni jinsi gani jina lako ni tukufu katika dunia yote, wewe ufunuaye utukufu wako juu mbinguni. 2 Kutoka katika midomo ya watoto na vichanga umeumba sifa kwa sababu ya utukufu wako, ili kuwanyamazisha maadui wote na walipa kisasi wote. 3 Ninapozitazama mbingu, ambazo vidole vyako vimeumba, mwezi na nyota, ambazo umeziweka kila mmoja katika nafasi yake, 4 Binadamu ni nani hata umtazame, na watu hata uwajali wao? 5 Umewaumba chini kidogo kuliko viumbe vya mbinguni na umewazunguka na utukufu na heshima. 6 Umemfanya binadamu kutawala kazi ya mikono yako; umeviweka vitu vyote chini ya miguu yake: 7 kondoo na ng'ombe wote, na hata wanyama wa porini, 8 ndege wa angani, na samaki wa baharini, na vyote vipitavyo katika mikondo ya bahari. 9 Yahweh Bwana wetu, ni jinsi gani jina lako ni tukufu katika dunia yote!

< Zaburi 8 >