< Zaburi 75 >

1 Tunatoa shukrani kwako, Mungu; tunatoa shukrani, maana wewe unaufunua uwepo wako; watu huzungumza kuhusu kazi zako za ajabu. 2 Kwa wakati maalum nitahukumu kwa haki. 3 Ingawa nchi na wenyeji wote watatikisika katika hofu, ninaifanyia nchi nguzo za kutosha. (Selah) 4 Nilisema kwa wenye kiburi, “Msiwe wenye kiburi,” na kwa waovu, “Msiinue mapembe. 5 Msiinue mapembe yenu kwenye marefu; wala msizungumze kwa shingo ya kiburi.” 6 Sio kutoka mashariki au magharibi, na wala sio kutoka jangwani ambako kuinuliwa kunakuja. 7 Bali Mungu ni muhumkumu; humshusha huyu na kumuinua huyu. 8 Kwa kuwa Yahwe kashikilia mkononi mwake kikombe cha mvinyo wenye povu, ambao umechanganywa na vilolezo, naye huimimina. Hakika waovu wote wa duniani watakunywa mvinyo hadi tone la mwisho. 9 Bali mimi nitaendelea kusema yale ambayo umeyatenda; nami nitamwimbia sifa Mungu wa Yakobo. 10 Yeye husema, “Nitayakata mapembe yote ya waovu, lakini mapembe ya wenye haki yatainuliwa.”

< Zaburi 75 >