< Zaburi 67 >

1 Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie (Selah) 2 ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote. 3 Watu wakusifu wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. 4 Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani. 5 Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. 6 Nchi imetoa mavuno yake na Mungu, Mungu wetu, ametubariki. 7 Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye.

< Zaburi 67 >