< Zaburi 65 >

1 Kwako wewe, Mungu katika Sayuni, sifa zetu za kungoja; viapo vyetu vitaletwa kwako. 2 Wewe usikiaye maombi yetu, miili yote itakuja kwako. 3 Maovu yanatutawala sisi; kama yalivyo makosa yetu, wewe utayasamehe. 4 Amebarikiwa mtu yule ambaye wewe huchagua kumsogeza karibu yako ili kwamba aishi hekaluni mwako. Tutatoshelezwa kwa uzuri wa nyumba yako, hekalu lako takatifu. 5 Katika haki wewe utatujibu sisi kwa kufanya mambo ya ajabu, Mungu wa wokovu wetu; wewe ambaye ni ujasiri wa mwisho wote wa nchi na wa wale walio mbali toka pande za bahari. 6 Kwa manaa ni wewe ndiye uliyeifanya milima imara, wewe ambaye umefungwa mkanda wa uweza. 7 Ni wewe unyamazishaye ngurumo za baharini; ngurumo za mawimbi yake, na vurugu za watu. 8 Wale wanaoishi sehemu za mwisho kabisa wa nchi wanaogopa ushahidi wa matendo yako; wewe hufanya mashariki na magharibi kushangilia. 9 Wewe huja kuisaidia nchi; unainyeshea inchi; wewe unaiimarisha nchi vizuri; mto wa Mungu umejaa maji; wewe humpa mwanadamu nafaka unapokuwa umekwisha iandaa nchi. 10 Wewe huyajaza matuta maji ya kutosha; wapasawazisha palipoinuka; wailainisha nchi kwa manyunyu ya mvua; waibariki mimea kati yao. 11 Umeuvika mwaka taji ya wema wako; mvumo wa mapito yako hudondosha unono katika nchi. 12 Majani ya nyikani hudondosha umande, na vilima vimevikwa furaha. 13 Malisho yamevishwa mifugo; mabonde pia yamefunikwa na nafaka; yanapiga kelele za shangwe, nayo yanaimba.

< Zaburi 65 >