< Zaburi 61 >

1 Sikia kulia kwangu, shughulikia maombi yangu. 2 Kutokea mwisho wa nchi nitakuita wewe wakati moyo wangu umeelemewa; uniongoze kwenye mwamba ulio juu kuliko mimi. 3 Maana wewe umekuwa kimbilio langu la usalama, nguzo imara dhidi ya adui. 4 Uniache niishi hemani mwako milele! Nipate kimbilio salama chini ya makazi ya mbawa zako. (Selah) 5 Kwa kuwa wewe, Mungu, umesikia viapo vyangu, wewe umenipa mimi urithi wa wale wanao liheshimu jina lako. 6 Wewe utaongeza maisha ya mfalme; miaka yake itakuwa kama vizazi vingi. 7 Yeye atabakia mbele ya Mungu milele. 8 Nitaliimbia sifa jina lako milele ili kwamba niweze kufanya viapo vyangu kila siku.

< Zaburi 61 >