< Zaburi 54 >

1 Uniokoe, Mungu, kwa jina lako, na kwa nguvu zako unihukumu. 2 Usikie maombi yangu, Mungu; uyategee sikio maneno ya mdomo wangu. 3 Kwa maana wageni wameinuka dhidi yangu, na watu wasio na huruma wanaitafuta roho yangu; nao hawakumuweka Mungu mbele yao. (Selah) 4 Tazama, Mungu ni msaidizi wangu; Bwana ndiye anisaidiaye. 5 Naye atawalipizia uovu maadui zangu; katika uaminifu wako, uwaharibu! 6 Nitakutolea dhabihu kwa moyo mkunjufu; nitalishukuru jina lako, Yahwe, kwa maana ni jema. 7 Kwa kuwa yeye ameniokoa katika kila shida; macho yangu yamewatazama adui zangu yakiwa na ushindi.

< Zaburi 54 >