< Zaburi 52 >

1 Kwa nini wewe unajivunia kufanya uovu, wewe mtu mwenye nguvu? Uaminifu wa agano la Mungu huja kila siku. 2 Ulimi wako hupanga uharibifu kama wembe mkali, na kufanya udanganyifu. 3 Wewe unapenda uovu kuliko wema na udanganifu kuliko kuongea haki. (Selah) 4 Wewe hupenda maneno ambayo huwaumiza wengine, wewe ulimi mdanganyifu. 5 Vivyo hivyo Mungu atakuadhibu wewe milele; yeye atakuchukua na kukuondoa katika hema yako na kukung'oa katika ardhi ya uhai. (Selah) 6 Wenye haki pia wataona na kuogopa; watamcheka na kusema, 7 “Tazama, huyu ni mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa kimbilio lake la usalama, bali aliamini katika wingi wa mali zake, naye alikuwa na nguvu alipowaharibu wengine.” 8 Lakini kwangu mimi, niko kama mti bora wa mzeituni katika nyumba ya Mungu; Nami nitaamini uaminifu wa agano la Mungu milele na milele. 9 Nitakushukuru wewe daima kwa uliyo tenda. Nitalisubiri jina lako, kwa sababu ni zuri, uweponi mwa wantu wako wa kimungu.

< Zaburi 52 >