< Zaburi 48 >

1 Yahwe ndiye aliye mkuu na mwenyekusifiwa sana, katika mji wa Mungu wetu kwenye mlima wake mtakatifu. 2 Ni mzuri katika mwinuko wake, furaha ya nchi yote, ni mlima Sayuni, kwenye upande wa kaskazini, mji wa Mfalme mkuu. 3 Mungu amejifunua mwenyewe katika jumba lake la kifahari kama kimbilio la usalama. 4 Maana, tazama, wafalme walikusanyika wenyewe; wote pamoja walipita. 5 Nao waliuona, wakashangaa; walifadhaika, na wakaharakisha kuondoka. 6 Pale pale tetemeko liliwashikilia, maumivu makali kama mwanamke anaye zaa. 7 Kwa upepo wa mashariki wewe huivunja meli ya Tarshishi. 8 Kama tulivyo sikia, vivyo hivyo tumeona katika mji wa Yahwe wa majeshi, katika mji wa Mungu wetu; Mungu atautunza milele. (Selah) 9 Tumeutafakari uaminifu wa agano lako, Mungu, katikati ya hekalu lako. 10 Kama lilivyo jina lako, Mungu, hivyo ndivyo zilivyo sifa zako mpaka miisho ya dunia; mkono wako wa kuume umejaa haki. 11 Milma Sayuni na ufurahi, nao wana wa Yuda washangilie kwa sababu ya amri ya haki yako. 12 Tembeeni katika Mlima Sayuni, muuzungukie mji, 13 mzitazame kwa makini nguzo zake, na mtazame majumba yake ya kifahari ili kwamba muweze kuwasimulia kizazi kijacho. 14 Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele; naye atakuwa kiongozi wetu mpaka kufa.

< Zaburi 48 >