< Zaburi 47 >

1 Pigeni makofi, enyi watu wote; mpigieni Mungu kelele za ushindi. 2 Kwa maana Yahwe Aliye Juu anatisha; ni Mfalme mkuu dunia yote. 3 Yeye anawatiisha chini yetu na mataifa chini ya miguu yetu. 4 Yeye huchagua urithi kwa ajili yetu, utukufu wa Yakobo ambaye alimpenda. Serah 5 Mungu ameinuliwa juu kwa shangwe, Kwa mbiu ya shangwe Yahwe yu juu. 6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa; mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa. 7 Kwa maana Mungu ni Mfalme duniani kote; mwimbieni mkiwa na uelewa. 8 Mungu anatawala mataifa yote; Mungu hukaa kwenye kiti cha enzi. 9 Wakuu wa watu wamekusanyika pamoja kwa watu wa Mungu wa Ibrahimu; kwa kuwa ngao za duniani ni za Mungu; yeye ameinuliwa juu sana.

< Zaburi 47 >