< Zaburi 46 >

1 Mungu kwetu ni kimbilio la usalama na nguvu, upatikanao tele wakati wa mateso. 2 Hivyo hatutaogopa, hata kama dunia italazimika kubadilika, hata kama milima italazimika kutetemeka na kuangukia kwenye mtima wa bahari, hata kama maji yatavuma kwa kishindo kikuu, 3 hata kama milima itatetemeka kwa vurugu ya maji. (Selah) 4 Kuna mto, mikondo yake huufanya mji wa Mungu kufurahi, mahali patakatifu pa hema ya Aliye Juu. 5 Mungu yuko katikati yake; naye hatasogezwa; Mungu atamsaidia, naye atafanya hivyo asubuhi na mapema. 6 Mataifa yalikasirika na falme zikataharuki; yeye alipaza sauti yake, na nchi ikayeyuka. 7 Yahwe wa majeshi yuko pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu la usalama. (Selah) 8 Njoni, mtazame matendo ya Yahwe, uharibifu alioufanya juu ya nchi. 9 Anaisitisha vita kwenye nchi; yeye anauvunja upinde na kuikata vipande vipande mishale; anazichoma ngao. 10 Mkae kimya na mjue kuwa mimi ni Mungu; nitainuliwa juu ya nchi. 11 Mungu wa majeshi yuko pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu la usalama. Serah

< Zaburi 46 >