< Zaburi 32 >

1 Zaburi ya Daudi. Zaburi. Amebarikiwa mtu yule aliyesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimesitiriwa. 2 Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe hamuhesabii hatia na ambaye rohoni mwake hamna udanganyifu. 3 Nilipokaa kimya, mifupa yangu ilidhohofika huku nikiugua muda wote. 4 Mchana na usiku mkono wako ulinielemea. nguvu zangu zilikauka wakati wa kiangazi. (Selah) 5 Ndipo nilipotambua makosa yangu kwako, nami sifichi tena uovu wangu. Nilisema, “Nitakiri makosa yangu kwa Yahwe,” nawe ulinisamehe hatia ya dhambi zangu. (Selah) 6 Kwa sababu ya haya, wale wote ambao ni wa kimungu wanapaswa kukuomba wakati wa shida kubwa. Nayo mafuriko yajapo, hayatawapata watu hao. 7 Wewe u mahali pangu pa kujifichia, nawe utanilinda matatizoni. Wewe utanizunguka pamoja na nyimbo zaushindi. (Selah) 8 Nitakuelekeza na kukufundisha katika njia upasayo kuiendea. Nitakuelekeza huku macho yangu yakikutazama. 9 Msiwe kama farasi au kama nyumbu, ambao hawana uelewa; ni kwa hatamu na lijamu tu unaweza kuwapeleka popote utakapo wao waende. 10 Waovu wanahuzuni nyingi, bali uaminifu wa agano la Yahwe utamzunguka yule anaye mwamini yeye. 11 Furahini katika Yahwe, na mshangilie, ninyi wenye haki; pigeni kelele za shangwe, ninyi nyote wenye haki mioyoni mwenu.

< Zaburi 32 >