< Zaburi 26 >

1 Unihukumu mimi, Yahwe, kwa kuwa nimeenenda katika uadilifu; nimeamini katika Yahwe bila kusita. 2 Unichunguze, Yahwe, na unijaribu; uujaribu usafi wa sehemu zangu za ndani na moyoni mwangu! 3 Kwa maana uaminifu wa agano lako uko mbele ya macho yangu, na mwenendo wangu ni katika uaminifu wako. 4 Mimi sichangamani na watu waovu, wala sichangamani na watu wanafiki. 5 Ninachukia waovu, na siishi na waovu. 6 Ninaosha mikono yangu kounesha sina hatia, na kuikaribia madhabahu yako, Yahwe, 7 kuimba wimbo wa sauti ya sifa na kutoa taarifa ya matendo yako yote ya ajabu. 8 Yahwe, ninaipenda nyumba ninayoishi, mahali ambapo utukufu wako unaishi! 9 Usiniangamize pamoja na wenye dhambi, au maisha yangu na watu wenye kiu ya kumwaga damu, 10 ambao katika mikono yao kuna njama, na ambao mkono wa kuume umejaa rushwa. 11 Lakini kwangu mimi, nitaenenda katika uadilifu; uniokoe na unihurumie. 12 Miguu yangu husimama sehemu salama; katika kusanyiko la watu nitambariki Yahwe!

< Zaburi 26 >