< Zaburi 24 >

1 Nchi ni ya Yahwe, na vyote viijazavyo, dunia, na wote wakaao ndani yake. 2 Kwa kuwa yeye aliianzisha juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito. 3 Ni nani atakaye panda mlima wa Yahwe? Ni nani atakaye simama patakatifu pake? 4 Yeye ambaye ana mikono misafi na moyo safi; ambaye hajauinua uongo, na haja apa kiapo ili kudanganya. 5 Yeye atapokea baraka kutoka kwa Yahwe na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake. 6 Kizazi cha wale wamtafutao Mungu ni kama hiki, wale ambao wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo. 7 Inueni vichwa vyenu, ninyi malango; muinuliwe juu, milango ya milango ya kudumu, ili kwamba Mfalme wa utukufu aweze kuingia! 8 Huyu Mfalme wa utukufu ni nani? Yahwe, mwenye nguvu na uweza; Yahwe, mwenye uweza katika vita. 9 Inueni vichwa vyenu, ninyi malango; muinuliwe juu, milango ya kudumu, ili kwamba Mfalme wa utukufu aweze kuingia! 10 Huyu Mfalme wa utukufu ni nani? Yahwe wa majeshi, yeye ni Mfalme wa utukufu.

< Zaburi 24 >