< Zaburi 20 >

1 Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mungu akusaidie wakati wa shida; na jina la Mungu wa Yakobo likulinde 2 na kutuma msaada kutoka mahali patakatifu kwa ajili ya kukutegemeza wewe kutoka Sayuni. 3 Naye akumbuke sadaka yako yote na kuipokea sadaka ya kuteketezwa. 4 Naye akujalie haja za moyo wako na kutimiza mipango yako yote. 5 Ndipo tutakapo shangilia katika ushindi wako, na, katika jina la Mungu wetu, tutapeperusha bendera. Yahwe naakupe maombi yako yote ya haki. 6 Sasa ninajua ya kuwa Yahwe atawaokoa wapakwa mafuta wake; yeye atamjibu yeye kutoka katika mbingu takatifu kwa uweza wa mkono wake wa kuume ambao waweza kumuokoa yeye. 7 Baadhi hamini katika magari na wengine katika farasi, lakini sisi tumuita Yahwe Mungu wetu. 8 Wao watashushwa chini na kuanguka, bali sisi tutainuka na kusimama wima! 9 Yahwe, umuokoe mfalme; utusaidie sisi tukuitapo.

< Zaburi 20 >