< Zaburi 18 >

1 Nakupenda, Yahwe, nguvu yangu. 2 Yahwe ni mwamba wangu, ngome yangu, yeye ambaye aniwekae kweye usalama; yeye ni Mungu wangu, mwamba wangu; ninapata kimbilio kwake. Yeye ni ngao yangu, pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu. 3 Nitamuita Yahwe kwa sababu anastahili kusifiwa, na nitaokolewa kutoka kwa adui zangu. 4 Kamba za mauti zilinizunguka, na mafuriko yakimbiayo yalinielemea. 5 Kamba za kuzimu zilinizunguka; mitego ya mauti ilininasa. (Sheol h7585) 6 dhiki yangu nilimuita Yahwe; Niliita msaada kwa Mungu. Naye alisikia sauti yangu kutoka hekaluni mwake; kuita kwangu msaada kulienda mpaka uweponi mwake; na kuingia masikioni pake. 7 Kisha nchi ikatikisika na kutetemeka; misingi ya milima pia ilitetemeka na kutikiswa kwa sababu Mungu alikuwa amekasirika. 8 Moshi ulifuka kutoka kwenye pua zake, na moto mkali ulitokea mdomoni mwake. Makaa yaliwashwa kwa moto huo. 9 Yeye alizifunua mbingu na alishuka chini, na giza nene lilikuwa chini ya miguu yake. 10 Alipanda kwenye kerubi na akaruka; alinyiririka kwenye mabawa ya upepo. 11 Yahwe alilifanya giza kuwa hema likimzunguka yeye, wingu la mvua zito katika mbingu. 12 Mawe ya barafu na makaa ya moto yalianguka kutoka katika mwangaza kabla yake. 13 Yahwe aliongea katika mbingu! Sauti ya aliye juu ilisikika. 14 Yeye aliifyatua mishale yake na kuwatawanya adui zake; na radi nyingi zenye mwanga alizitawanya katika maeneo tofauti tofauti. 15 Ndipo mifereji ya maji ilitokea; misingi ya dunia ikadhihirishwa kwa mlio wa pigo lako, Yahwe kwa sauti ya pumzi ya pua zako. 16 Yeye alishuka chini kutokea juu; akanishikilia mimi! Akanivuta nje ya maji yafurikayo. 17 Aliniokoa kutoka kwa maadui zangu wenye nguvu, kutoka kwa wale ambao walinichukia mimi, kwa kuwa walikuwa na nguvu sana kuliko mimi. 18 Wao walikuja kinyume na mimi katika siku ile ya dhiki yangu lakini Mungu alikuwa msaada wangu! 19 Yeye aliniweka huru katika eneo pana la wazi; yeye aliniokoa kwa sababu alipenezwa nami. 20 Yahwe amenitunuku mimi kwa sababu ya haki yangu; yeye amenirejesha mimi kwa sababu mikono yangu ilikuwa misafi. 21 Kwa kuwa nimezitunza njia za Yahwe na sijafanya uovu wa kumgeuka Mungu wangu. 22 Kwa kuwa amri zake zote za haki zimekuwa mbele yangu; kama asemavyo, sijaenda kinyume nazo. 23 Pia nimekuwa sina hatia mbele zake, na nimejiweka mwenyewe mbali na dhambi. 24 Hivyo Yahwe amenirejesha kwa sababu ya haki yangu, na kwa sababu mikono yangu ilikuwa safi mbele ya macho yake. 25 Kwa yeyote aliye mwaminifu, jionyeshe wenyewe kuwa mwaminifu; kwa mtu asiye na lawama, jionyeshe mwenyewe kuwa usiye na lawama. 26 Kwa yeyote aliye msafi, jionyeshe mwenyewe safi; bali ni mjanja kwa yeyote aliye geuzwa. 27 Kwa kuwa wewe huwaokoa watu walio taabishwa, lakini wewe huwashusha chini wale wenye majivuno, yaani macho yaliyo jinua! 28 Kwa kuwa wewe huipa mwanga taa yangu; Yahwe Mungu wangu hutia mwanga giza langu. 29 Kwa kuwa kwa kupitia wewe ninaweza kuruka juu ya kiwazo kilichowekwa; kupitia Mungu ninaweza kuruka juu ya ukuta. 30 Kama kwa Mungu: njia yake ni kamilifu. Neno la Yahwe ni safi! Yeye ni ngao kwa yeyote anaye kimbilia katika yeye. 31 Kwa kuwa nani ni Mungu ispokuwa Yahwe? Nani ndiye mwamba ispokuwa Mungu wetu? 32 Ni Mungu anitiaye nguvu ndani yangu kama vile mkanda, ambaye humweka mtu mwenye lawama katika njia yake. 33 Yeye hunifanya miguu yangu kuwa myepesi kama mbawala na kuniweka mahali pa juu! 34 Yeye hufunza viganja vyangu kwa ajili ya vita na mikono yangu kupiga upinde wa shaba. 35 Wewe umenipa mimi ngao ya wokovu. Mkono wako wa kuume umenisaidia, na neema yako imenifanya kuwa mkubwa. 36 Wewe umetengeneza nafasi pana kwa ajili ya miguu yangu ili miguu yangu isiteleze. 37 Ninawashawishi adui zangu na kuwakamata; nami sikurudi nyuma mpaka walipo haribiwa. 38 Niliwashambulia hata hawakuweza kuamka; nao wameangukia chini ya miguu yangu. 39 Kwa kuwa unanitia nguvu kama mshipi kwa ajili ya vita; wewe unawaweka chini yangu wale ambao wanainuka kinyume na mimi. 40 Wewe ulinipa visogo vya maadui zangu; niliwaagamiza wale walio nichukia. 41 Wao waliita msaada lakini hakuna aliye wasaidia; walimuita Yahwe, lakini hakuwaitikia. 42 Niliwapiga wao katika vipande vidogo vidogo kama vile vumbi mbele ya upepo; niliwatupa nje kama udongo mtaani. 43 Wewe uliniokoa mimi kutoka katika migogoro ya watu. wewe umenifanya kichwa juu ya mataifa. Watu ambao sikuwahi kuwafahamu huntumikia. 44 Pindi tu waliposikia kuhusu mimi, wao walinitii; wageni walilazimishwa kunisujudu. 45 Wageni walitoka kwenye ngome yao wakitetemeka. 46 Yahwe anaishi; mwamba wangu usifiwe. Ainuliwe Mungu wa wokovu wangu. 47 Yeye ni Mungu ambaye hutelekeza visasi kwa ajili yangu, ambaye huwatiisha mataifa chini yangu. 48 Nimewekwa huru kutoka kwa adui zangu! wewe uliniinua juu ya wale walioinuka kunyume na mimi! Wewe uliniokoa kutoka kwa watu wenye vurugu. 49 Kwa hiyo nitakushukuru wewe, Yahwe, kati ya mataifa; Nitaliimbia sifa jina lako! 50 Mungu hutoa ushindi mkuu kwa mfalme wake, na yeye huonyesha uaminifu wa agano lake kwa mpakwa mafuta wake, kwa Daudi na ukoo wake milele.

< Zaburi 18 >