< Zaburi 150 >

1 Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe katika patakatifu pake; msifuni katika mbingu za ukuu wake. 2 Msifuni yeye kwa matendo yake makuu; msifuni yeye kwa kadri ya wingi wa ukuu wake. 3 Msifuni kwa mlipuko wa pembe; msifuni kwa kinanda na kinubi. 4 Msifuni kwa ngoma na kucheza; msifuni kwa vyombo vya nyuzi na filimbi. 5 Msifuni kwa matoazi yavumayo; msifuni kwa matoazi avumayo sana. 6 Kila kilicho na pumzi kimsifu Yahwe. Msifuni Yahwe.

< Zaburi 150 >