< Zaburi 149 >

1 Msifuni Yahwe. Mwimbieni Yahwe wimbo mpya; imbeni sifa zake katika kusanyiko la waaminifu. 2 Israeli ishangilie katika yeye aliye iumba; watu wa Sayuni na washangilie katika mfalme wao. 3 Nao walisifu jina lake kwa kucheza; na wamuimbie sifa yeye kwa ngoma na kinubi. 4 Kwa kuwa Yahwe hupata furaha katika watu wake; huwapa utukufu wanyeyekevu kwa wokovu. 5 Wacha Mungu wauchangilie ushindi; nao waimbe kwa furaha vitandani mwao. 6 Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na panga mbili zenye makali mkononi mwao 7 kutekeleza kisasi juu ya mataifa na matendo ya adhabu juu ya watu. 8 Nao watawafunga wafalme wao kwa minyororo na wakuu wao kwa pingu za chuma. Watatekeleza hukumu ambayo imeandikwa. 9 Hii itakuwa ni heshima kwa ajili ya watakatifu wake wote. Msifuni Yahwe.

< Zaburi 149 >