< Zaburi 146 >

1 Msifu Yahwe. Msifu Yahwe, ee nafsi yangu. 2 Ninamsifu Mungu maisha yangu yote; nitamuimbia sifa Mungu wangu ni ngali ni hai. 3 Msiweke imani katika wakuu au wanadamu, ambaye katika yeye hamna wokovu. 4 Wakati uhai wa pumzi ya mtu unapokoma, hurudi aridhini; siku hiyo mipango yake hufikia mwisho. 5 Amebarikiwa yule ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake liko katika Yahwe Mungu wake. 6 Yahwe aliumba mbingu na nchi, bahari, na vyote vilivyomo; huitazama kweli milele. 7 Yeye hutekeleza hukumu kwa ajili ya walioonewa na huwapa chakula wenye njaa. Yahwe huwafungua waliofungwa; 8 Yahwe huyafungua macho ya kipofu; Yahwe huwainua walioinama; Yahwe huwapenda watu wenye haki. 9 Yahwe huwalinda wageni katika nchi; huwainua yatima na wajane, bali huipinga njia ya wasio haki. 10 Yahwe atatawala milele, Mungu wako, Sayuni, kwa vizazi vyote. Msifuni Yahwe.

< Zaburi 146 >