< Zaburi 137 >

1 Kando ya mito ya Babeli tuliketi na tulilia tulipokumbuka kuhusu Sayuni. 2 Tulitundika vinubi vyetu kwenye miti ya Babylon. 3 Huko watekaji wetu walitaka tuwaimbie, na wale walio tudhihaki walitutaka sisi tufurahi, wakisema, “Tuimbieni moja ya nyimbo za Sayuni.” 4 Tungewezaje kuimba wimbo unaomuhusu Yahwe katika nchi ya ugeni? 5 Kama nikikusahau wewe, Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake. 6 Ulimi wangu na ushikamane juu ya kinywa changu kama nisipokufikiria tena, na kama sipendelei zaidi Yerusalemu kuliko furaha yangu kuu. 7 Kumbuka, Ee Yahwe, kile walichofanya Waedomu siku ya anguko la Yerusalemu. Walisema, “Ibomoeni, ibomoeni mpaka chini kwenye misingi yake.” 8 Binti za Babeli, hivi karibuni wataharibiwa- mtu na abalikiwe, yeyote atakaye walipizia yale mliotufanyia sisi. 9 Mtu na abarikiwe, yeyote achukuaye na kusambaratisha watoto wenu juu ya jiwe.

< Zaburi 137 >