< Zaburi 133 >

1 Tazama, jinsi ilivyo vema na yakupendeza ndugu waishi pamoja, kwa umoja! 2 Ni kama mafuta mazuri kichwani yashukayo ndevuni. Ndevu za Haruni, na yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. 3 Ni kama umande wa Hermoni uangukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko Bwana alipoamuru baraka, naam uzima milele na milele.

< Zaburi 133 >