< Zaburi 131 >

1 Yahwe, moyo wangu haujivuni wala macho yangu hayana kuburi. Sina matarajio makubwa kwa ajili yangu mwenyewe wala kujihofia kwa mambo ambayo yako juu ya uwezo wangu. 2 Hakika nimejituliza na kuinyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa na mama yake, nafsi yangu ndani yangu iko kama mtoto aliye achishwa. 3 Israeli, umtumainie Yahwe sasa na hata milele.

< Zaburi 131 >