< Zaburi 130 >

1 Toka ndani yangu ninakulilia, Yahwe. 2 Bwana, usikie sauti yangu; masikio yako na yasikie kwa makini kuomba kwangu kwa ajili ya huruma. 3 Kama wewe, Yahwe, ungehesabu maovu, Bwana, ni nani angesimama? 4 Lakini kwako kuna msamaha, ili uweze kuheshimiwa. 5 Ninamngoja Yahwe, nafsi yangu inasubiri, na katika neno lake ninatumainia. 6 Nafsi yangu inamngoja Bwana kuliko mlinzi aingojavyo asubuhi. 7 Israeli, umtumainie yahwe. Yahwe ni wenye huruma, na yuko tayari kusamehe. 8 Ni yeye ambaye ataikomboa istaeli dhidi ya dhambi zake zote.

< Zaburi 130 >