< Zaburi 126 >

1 Bwana alipowarejesha mateka wa Sayuni, tulikuwa kama waotao ndoto. 2 Vinywa vyetu vilijawa na vicheko na ndimi zetu zilijawa na kuimba. Kisha wakasema kati ya mataifa, “Yahwe amewatendea mambo makuu.” 3 Yahwe alitufanyia mambo makuu; ni furaha gani tuliyokuwa nayo! 4 Ee Yahwe, uwarejeshe mateka wetu, kama vijito vya kusini. 5 Wale wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha. 6 Yeye aendaye akilia, akibeba mbegu kwa ajili a kupanda, atarudi tena kwa kelele za furaha, akileta miganda yake.

< Zaburi 126 >