< Zaburi 122 >

1 Nilifurahi waliponiambia, “Na twende kwenye Nyumba ya Yahwe.” 2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama ndani ya malango yako! 3 Ee Yerusalemu, uliojengwa kama mji uliopangiliwa kwa umakini! 4 Makabila huenda juu Yerusalemu, makabila ya Yahwe; kama ushuhuda wa Israeli, kulishukuru jina la Yahwe. 5 Huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi. 6 Ombeni kwa ajili ya amani ya Yerusalemu! “Wote wakupendao wawe na amani. 7 Amani iwepo ndani ya kuta zako ili ikutetee, na wawe na amani ndani ya ngome zako.” 8 Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu nitasema, “Amani iwe ndani yenu.” 9 Kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu, nitatafuta mema kwa ajili yako.

< Zaburi 122 >