< Zaburi 121 >

1 Nitayainua macho yangu nitazame milimani. Msaada wangu utatoka wapi? 2 Msaada wangu unatoka kwa Yahwe, aliyezifanya mbingu na nchi. 3 Hatauacha mguu wako uteleze; yeye akulindaye hatasinzia. 4 Tazama, mlinzi wa Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi kamwe. 5 Yahwe ni mlinzi wako; Yahwe ni uvuli mkono wako wa kuume. 6 Jua halitakudhuru wakati wa mchana, wala mwezi wakati wa usiku. 7 Yahwe atakulinda na madhara yote, na ataulinda uhai wako. 8 Yahwe atakulinda katika yote ufanyayo sasa na hata milele.

< Zaburi 121 >