< Zaburi 120 >

1 Katika dhiki yangu nilimuita Yahwe, naye akanijibu. 2 Uiokoe nasfi yangu, yahwe, dhidi ya wale wadanganyao kwa midomo yao na wanenao hila kwa ndimi zao. 3 Yahwe atawaadhibu vipi, na atawafanyia kitu gani zaidi, ninyi mlio na ulimi mdanganyifu? 4 Atawaadhibu kwa mishale ya shujaa iliyo nolewa kwa makaa ya moto ya mretemu. 5 Ole wangu mimi kwa sababu ninaishi kwa muda Mesheki; huko nyuma niliishi kati ya maskani ya Kedari. 6 Kwa muda mrefu sana niliisha na wale waichukiao amani. 7 Nipo kwa ajili ya amani, lakini ninenapo, wao wako kwa ajili ya vita.

< Zaburi 120 >