< Zaburi 114 >

1 Israeli ilipotoka Misri, na nyumba ya Yakobo toka kutoka katika wale watu wa kigeni, 2 Yuda ilifanyika kuwa mahali pake patakatifu, Ufalme wa Israeli. 3 Bahari iliona ikakimbia; Yordani ilirudi nyuma. 4 Milima iliruka kama kondoo waume, vilima viliruka kama wana-kondoo. 5 Ewe Bahari kwa nini ulikimbia? Yordani kwa nini ulirudi nyuma? 6 Milima, kwa nini uliruka kama kondoo waume? Enyi vilima wadogo, kwa nini mliruka kama wana-kondoo? 7 Tetemeka, ee nchi, mbele za Bwana, uweponi mwa Mungu wa Yakobo. 8 Aligeuza mwamba kuwa ziwa la maji, jiwe gumu kuwa chemchem.

< Zaburi 114 >