< Zaburi 113 >

1 Msifuni Yahwe. Msifuni yeye, enyi watumishi wa Yahwe; lisifuni jina la Yahwe. 2 Litukuzwe jina la Yahwe, tangu sasa na hata milele. 3 Toka maawio ya jua hata machweo yake, Jina la Yahwe lazima lisifiwe. 4 Yahwe ameinuliwa juu ya mataifa yote, na utukufu wake wafika juu mbinguni. 5 Ni nani aliye kama Yahwe Mungu wetu, aliye na kiti chake juu, 6 atazamaye chini angani na duniani? 7 Humwinua maskini toka mavumbini na kumpandisha muhitaji kutoka jaani, 8 ili amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. 9 Humpa watoto wanamke aliye tasa, humfanya yeye kuwa mama wa watoto mwenye furaha. Msifuni Yahwe!

< Zaburi 113 >