< Zaburi 111 >

1 Msifuni Yahwe. Nitamshukuru Yahwe kwa moyo wangu wote katikati ya kusanyiko la wanye haki, na katika mkutano. 2 Kazi za Yahwe ni kuu, zikisubiriwa na wale wazitamanio. 3 Kazi yake ni adhama na utukufu, na haki yake yadumu milele. 4 Hufanya mambo makuu ambayo yatakumbukwa; Yahwe ni mwenye huruma na neema. 5 Huwapa chakula wafuasi wake waaminifu. Siku zote atalikumbuka agano lake. 6 Alionesha uweza wa kazi zake kwa watu wake kwa kuwapa urithi wa mataifa. 7 Kazi za mikono yake ni za kuaminika na haki; maagizo yake yote ni ya kuaminika. 8 Yamethibitika milele, yamefanywa katika uaminifu na vizuri. 9 Aliwapa ushindi watu wake; aliliteuwa agano lake milele; jina lake ni takatifu na lakutisha. 10 Kumcha Yahwe ni mwanzo wa hekima; wale washikao maagizo yake wana uelewa mzuri. Sifa yake yadumu milele.

< Zaburi 111 >