< Zaburi 110 >

1 Yahwe humwambia bwana wangu, “Kaa mkono wangu wa kuume mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” 2 Yahwe atainyosha fimbo ya nguvu yako toka Sayuni; utawale kati ya adui zako. 3 Siku ile ya uweza wako watu wako watakufuata wakiwa katika mavazi matakatifu ya hiari yao wenyewe; tokea tumbo la alfajiri ujana wako utakuwa kwako kama umande. 4 Yahwe ameapa, na hatabadilika: “Wewe ni kuhani milele, baada ya namna ya Melkizedeki.” 5 Bwana yuko mkono wako wa kuume. Siku ile ya hasira yake atawaua wafalme. 6 Yeye atahukumu matifa; ataujaza uwanja wa vita kwa maiti; atawauwa viongozi kaitka nchi nyingi. 7 Atakunywa maji ya kijito njiani, kisha baada ya ushindi atainua kichwa chake juu.

< Zaburi 110 >