< Zaburi 11 >

1 Ni kwako Yahweh ninapata usalama; ni kwa namna gani utasema na mimi, “Ruka kama ndege hadi mlimani”? 2 Tazama! Waovu wana andaa pinde zao. Wana tayarisha gizani mishale yao kwenye kamba ili kufyatua mioyo ya wenye haki. 3 Ikiwa misingi imeharibiwa, mwenye haki atafanya nini? 4 Yahweh yuko katika hekalu takatifu; macho yake yanatazama, yakiuchunguza ubinadamu. 5 Yahweh huwachunguza wote wenye haki na waovu, bali huwachukia wapendao kuwaumiza wengine. 6 Yeye huwanyeshea waovu makaa ya mawe na moto wa jehanamu; upepo uunguzao utakuwa ni sehemu yao kutoka katika kikombe chake! 7 Kwa kuwa Yahweh ni mwenye haki, Naye hupenda haki; wenye haki watauona uso wake.

< Zaburi 11 >