< Zaburi 109 >

1 Zaburi ya Daudi. Mungu ninaye msifu, usinyamaze kimya.
למנצח לדוד מזמור אלהי תהלתי אל תחרש׃
2 Kwa maana waovu na wadanganyifu wananishambulia; wanazungumza uongo dhidi yangu.
כי פי רשע ופי מרמה עלי פתחו דברו אתי לשון שקר׃
3 Wananizunguka na kusema mambo ya chuki, na wananishambulia bila sababu.
ודברי שנאה סבבוני וילחמוני חנם׃
4 Wananilipa kashfa badala ya upendo, lakini mimi ninawaombea.
תחת אהבתי ישטנוני ואני תפלה׃
5 Wananilipa uovu badala ya mema, na wanachukia upendo wangu.
וישימו עלי רעה תחת טובה ושנאה תחת אהבתי׃
6 Teua mtu mwovu aliye adui zaidi kama watu hawa; teua mshitaki asimame mkono wake wa kuume.
הפקד עליו רשע ושטן יעמד על ימינו׃
7 Na atakapohukumiwa, aonekane na hatia; maombi yake yachukuliwe kuwa ni dhambi.
בהשפטו יצא רשע ותפלתו תהיה לחטאה׃
8 Siku zake na ziwe chahe; mamlaka yake na yachukuliwe na mtu mwingine.
יהיו ימיו מעטים פקדתו יקח אחר׃
9 Watoto wake wawe yatima, na mke wake awe mjane.
יהיו בניו יתומים ואשתו אלמנה׃
10 Watoto wake wenye kutanga tanga na kuombaomba, wakiondoka katika nyumba zao zilizo haribika na kuomba chakula au pesa kwa wapita njia.
ונוע ינועו בניו ושאלו ודרשו מחרבותיהם׃
11 Mdai na achukue vitu vyake vyote amilikivyo; wageni wateke mapato ya kazi yake.
ינקש נושה לכל אשר לו ויבזו זרים יגיעו׃
12 Asiwepo mtu yeyote wa kumfanyia wema; mtu yeyote asiwahurumie yatima wake.
אל יהי לו משך חסד ואל יהי חונן ליתומיו׃
13 Watoto wake waangamizwe; majina yao na yafutwe katika kizazi kijacho.
יהי אחריתו להכרית בדור אחר ימח שמם׃
14 Uovu wa baba zake utajwe kwa Yahwe; na dhambi ya mama yake isisahaulike.
יזכר עון אבתיו אל יהוה וחטאת אמו אל תמח׃
15 Hatia zao na ziwe mbele ya Yahwe siku zote; Yahwe na aiondoe kumbukumbu yao duniani.
יהיו נגד יהוה תמיד ויכרת מארץ זכרם׃
16 Yahwe na afanye hivi kwa sababu mtu huyu kamwe hakusumbuka kuonesha uaminifu wa agano wowote, lakini badala yake aliwasumbua wanyonge, wahitaji, na kuwaua walio vunjika moyo.
יען אשר לא זכר עשות חסד וירדף איש עני ואביון ונכאה לבב למותת׃
17 Alipenda kulaani; na imrudie juu yake. Alichukia kubariki; baraka zozote na zisije kwake.
ויאהב קללה ותבואהו ולא חפץ בברכה ותרחק ממנו׃
18 Alijivika kulaani kana kwamba ni vazi lake, na laana yake iliingia ndani yake kama maji, na kama mafuta mifupani mwake.
וילבש קללה כמדו ותבא כמים בקרבו וכשמן בעצמותיו׃
19 Laana zake na ziwe kwake kama vazi avaalo kujifunika mwenyewe, na kama mkanda avaao kila siku.
תהי לו כבגד יעטה ולמזח תמיד יחגרה׃
20 Na haya yawe malipo ya mshitaki wangu kutoka kwa Yahwe, ya wale wasemao mambo maovu juu yangu.
זאת פעלת שטני מאת יהוה והדברים רע על נפשי׃
21 Yahwe Bwana wangu, unishughulikie kwa wema kwa ajili ya jina lako. Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni mwema, uniokoe.
ואתה יהוה אדני עשה אתי למען שמך כי טוב חסדך הצילני׃
22 Kwa maana ni mnyonge na muhitaji, na moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.
כי עני ואביון אנכי ולבי חלל בקרבי׃
23 Ninatoweka kama kivuli cha jioni; ninapeperushwa kama nzige.
כצל כנטותו נהלכתי ננערתי כארבה׃
24 Magoti yangu ni dhaifu kutokana na kufunga; ninakuwa mwembamba na mifupa.
ברכי כשלו מצום ובשרי כחש משמן׃
25 Nimedharauliwa na washitaki wangu; wanionapo; hutikisa vichwa vyao.
ואני הייתי חרפה להם יראוני יניעון ראשם׃
26 Nisaidie, Yahwe Mungu wangu; uniokoe kwa uaminifu wa agano lako.
עזרני יהוה אלהי הושיעני כחסדך׃
27 Nao wajue kuwa wewe umefanya haya, kwamba wewe, Yahwe, umetenda haya.
וידעו כי ידך זאת אתה יהוה עשיתה׃
28 Ingawa wananilaani, tafadhali unibariki; wanishambuliapo, waaibishwe, lakini mtumishi wako afurahi.
יקללו המה ואתה תברך קמו ויבשו ועבדך ישמח׃
29 Washitaki wangu na wavishwe kwa aibu; wavae aibu yao kama vazi.
ילבשו שוטני כלמה ויעטו כמעיל בשתם׃
30 Kwa kinywa changu ninatoa shukrani kuu kwa Yahwe; nitamsifu yeye katikati ya kusanyiko.
אודה יהוה מאד בפי ובתוך רבים אהללנו׃
31 Maana nitasimama mkono wa kuume wa mhitaji, ili nimuokoe dhidi ya wale wanao muhukumu.
כי יעמד לימין אביון להושיע משפטי נפשו׃

< Zaburi 109 >