< Zaburi 108 >

1 Ee Mungu, moyo wangu u thabiti; nitaimba, naam, nitaimba sifa pia kwa moyo mkuu. 2 Amka, kinanda na kinubi; nitaamka alfajiri. 3 Nitakushukuru wewe, Yahwe, kati ya watu; nitakuimbia sifa kati ya mataifa. 4 Kwa maana uaminifu wa agano lako ni mkuu juu ya mbingu; na uaminifu wako wafika mawinguni. 5 Ee Mungu, uinuliwe, juu ya mbingu, na utukufu wako utukuke juu ya nchi. 6 Ili kwamba wale uwapendao waokolewe, utuokoe sisi kwa mkono wako wa kuume na unijibu. 7 Mungu ameongea katika utakatifu wake; “Nitashangilia; nitaigawanya Shekemu na nitalipima bonde la Sukothi. 8 Gileadi ni yangu, na manase ni yangu; Ephraimu ni nguvu ya kichwa changu; Yuda ni fimbo yangu ya kifalme. 9 Moabu ni bakuli langu la kunawia; nitatupa kiatu changu juu ya Edomu; nitapaza sauti katika ushindi kwa ajili ya Filisti. 10 Ni nani atakaye nipeleka kwenye mji imara? Ni nani atakayeniongoza mpaka Edomu?” 11 Ee Mungu, sio wewe uliyetukataa? Hauendi vitani na jeshi letu. 12 Utupe msaada dhidi ya adui yetu, maana msaada wa wanadamu ni bure. 13 Tutashinda kwa msaada wa Mungu; atawakanyaga kwa adui zetu.

< Zaburi 108 >