< Zaburi 101 >

1 Nitaimba uaminifu wa agano lako na hukumu; kwako, Ee Yahwe, Nitakuimbia sifa. 2 Nitatembea katika njia ya uadilifu. Oh, ni lini utakuja kwangu? Nitatembea kwa uadilifu ndani ya nyumba yangu. 3 Sitaweka matendo maovu mbele ya macho yangu; ninachukia uovu usio na maana; hauta shikamana nami. 4 Watu waliopotoka wataniacha mimi; mimi sichangamani na uovu. 5 Nitamwangamiza yeyote amsengenyaye jirani yake kwa siri. Sitamvumilia yeyote mwenye kiburi. 6 Nitawachagua walio waaminifu katika nchi wakae upande wangu. Wale watembeao katika njia ya uhadilifu watanitumikia. 7 Watu wadanganyifu hawatabaki ndani ya nyumba yangu; waongo hawatakaribishwa mbele ya macho yangu. 8 Asubuhi hata asubuhi nitawaangamiza waovu wote kutoka nchini; nitawaondoa watendao maovu wote katika mji wa Yahwe.

< Zaburi 101 >