< Zaburi 100 >

1 Mpigieni Yahwe kelele za furaha, enyi nchi yote. 2 Mtumikieni Yahwe kwa furaha; njoni mbele zake mkiimba kwa furaha. 3 Mjue kuwa Yahwe ni Mungu; alituumba, na sisi tu wake. Tu watu wake na kondoo wa malisho yake. 4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na nyuani mwake kwa kusifu. Mshukuruni yeye na litukuzeni jina lake. 5 Maana Yahwe ni mwema; uaminifu wa agano lake wadumu milele na uaminifu wake vizazi na vizazi vyote.

< Zaburi 100 >