< Mithali 6 >

1 Mwanangu, kama utaweka pesa zako kuwa dhamana kwa mkopo wa jirani yako; kama ukitoa ahadi yako katika mkopo wa mtu usiyemjua, 2 basi umejiwekea mtego mwenyewe na umenaswa kwa maneno ya kinywa chako. 3 Mwanagu, ukinaswa kwa maneno yako mwenyewe, fanya haya ili kujiokoa, kwa kuwa umeangukia kwenye mikono ya jirani yako; nenda unyenyekee na ufanye shauri mbele ya jirani yako. 4 Usiruhusu usingizi katika macho yako wala kope za macho yako kusinzia. 5 Jiokoe mwenyewe kama swala kutoka katika mkono wa mwindaji, kama ndege kutoka katika mkono wa mwinda ndege. 6 Wewe mtu mvivu, mwangalie mchwa, zitafakari njia zake ili kupata busara. 7 Hana akida, afisa au mtawala, 8 lakini huandaa chakula chake wakati wa joto na wakati wa mavuno huweka hazina ili kula baadaye. 9 Ewe mtu mvivu, utalala hata lini? Wakati gani utainuka usingizini?” 10 Lala kidogo, sizia kidogo, kunja mikono kupumzika kidogo” - 11 ndipo umasikini wako utakapokujia kama mporaji na uhitaji wako kama askari wa vita. 12 Mtu asiyefaa-mtu mwovu- huishi kwa kauli za udanganyifu wake, 13 akipepesa macho yake, akiashilia kwa miguu yake na kusonta kwa videle vyake. 14 Hufanya njama za uovu kwa hila ya moyo wake; daima huchochea faraka. 15 Kwa hiyo msiba wake utamkumba kwa ghafula, punde atavunjika vibaya wala hatapona. 16 Kuna vitu sita ambavyo Yehova huvichukia, saba ambavyo ni chukizo kwake. 17 Macho ya mtu mwenye kiburi, ulimi wa uongo, mikono inayomwaga damu ya watu maasumu, 18 moyo unaobuni njama mbaya, miguu inayokimbilia maovu upesi, 19 shahidi asemaye uongo na apandaye faraka kati ya ndugu. 20 Mwanangu, itii amri ya baba yako na wala usiyaache mafundisho ya mama yako. 21 Uyafunge katika moyo wako siku zote; yafunge kwenye shingo yako. 22 utembeapo, yatakuongoza; ulalapo yatakulinda, na uamkapo yatakufundisha. 23 Maana amri ni taa, na mafundisho ni nuru; kinga za kuadilisha za njia ya uzima. 24 Yanakulinda dhidi ya mwanamke malaya, dhidi ya maneno laini ya uzinzi. 25 Moyoni mwako usiutamani uzuri wake wala usitekwe katika kope zake. 26 Kulala na malaya inaweza kugharimu bei ya kipande cha mkate, lakini mke wa mtu mwingine inagharimu uzima wako wote. 27 Je mtu anaweza kubeba moto katika kifua chake bila kuuguza mavazi yake? 28 Je mtu anaweza kutembea juu ya makaa bila kuchomwa miguu yake? 29 Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa jirani yake; yule alalaye na huyo mke hatakosa adhabu. 30 Watu hawawezi kumdharau mwizi kama anaiba ili kukidhi hitaji lake la njaa. 31 Walakini akimatwa, atalipa mara saba ya kile alichoiba; lazima atoe kila kitu cha thamani katika nyumba yake. 32 Mtu anayefanya uzinzi hana akili; hufanya hiyo kwa uharibifu wake mwenyewe. 33 Anasitahili aibu na majeraha na fedheha yake haiwezi kuondolewa. 34 Maana vivu humghadhibisha mtu; hatakuwa na huruma wakati wa kulipa kisasi chake. 35 Ujapompa zawadi nyingi, hatakubali mbadala wa kusuruhishwa wala kulipwa.

< Mithali 6 >