< Mithali 26 >

1 Kama theluji wakati wa joto au mvua kwenye mavuno, ndivyo mpumbavu asivyostahili heshima. 2 Kama shorowanda hurukaruka na kumeza wadudu wakati wa kuruka, ndivyo ilivyo laana isiyostahili haishuki. 3 Mjeledi ni kwa ajili ya farasi, hatamu kwa ajili ya punda na fimbo ni kwa ajili mgongo wa wapumbavu. 4 Usimjibu mpumbavu na kujiunga katika upumbavu wake, au utakuwa kama yeye. 5 Mjibu mpumbavu na jiunge katika upumbavu wake, ili asiweze kuwa na busara katika macho yake mwenyewe. 6 Anayetuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu huikata miguu yake mwenyewe na kunywa vurugu. 7 Miguu ya kiwete inayoning'ia chini ni kama mithali kwenye kinywa cha wapumbavu. 8 Kujaribisha jiwe kwenye kombeo ni sawa na kumpa heshima mpumbavu. 9 Mwiba unaochoma kwenye mkono wa mlevi ni kama mithali kwenye kinywa cha wapumbavu. 10 Mpiga mishale anayejeruhi kila mtu ni kama mtu anayemwajiri mpumbavu au kila mtu anayepita karibu yake. 11 Kama mbwa anavyorudia matapishi yake, ndivyo alivyo mpumbavu anayerudia upuuzi wake. 12 Je unamwona mtu mwenye busara katika macho yake mwenyewe? Mpumbavu anamatumaini zaidi kuliko yeye. 13 Mtu mvivu husema “Kuna simba kwenye barabara! Kuna simba katikati ya njia kuu!” 14 Kama mlango unavyogeuka kwenye bawaba zake, ndivyo alivyo mtu mvivu kwenye kitanda chake. 15 Mtu mvivu hutia mkono wake kwenye sufuria na bado hana nguvu kuunyanyua kwenda kwenye kinywa chake. 16 Mtu mvivu ni mwenye hekima kwenye macho yake mwenyewe kuliko watu saba wenye ufahamu. 17 Kama mtu anayeshikilia masikio ya mbwa, ndivyo alivyo mpitajia anayepata hasira kwenye ugomvi ambao si wake. 18 Kama mtu mwendawazimu anayetupa mishale, 19 ndivyo alivyo ambaye humdanganya jirani yake na kusema, “Je sikuwa naongea utani?” 20 Kwa kukosa kuni, moto huzimika; na pale pasipo na mmbea ugomvi hukoma. 21 Mkaa ni kwa kuwasha makaa na kuni kwa ajili ya moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuwasha ugomvi. 22 Maneno ya mmbea ni kama chembe tamu; nazo zinashuka chini kwenye sehemu za ndani ya mwili. 23 Kioo kinachofunika chombo cha udongo ni kama midomo inayoungua na moyo mbaya. 24 Yule ambaye huwachukia wengine huficha hisia zake kwa midomo na hufunika uongo ndani yake mwenyewe. 25 Ataongea kwa huruma, lakini usimwamini, maana kuna machukizo saba kwenye moyo wake. 26 Ingawa chuki zake zimefunikwa kwa udanganyifu, uovu wake utakuwa wazi katika kusanyiko. 27 Anayechimba shimo atatumbukia ndani yake na jiwe litamsaga yule anayelisukuma. 28 Ulimi wa uongo huchukia watu unaowajeruhi na kinywa cha uongo husogeza karibu uharibifu.

< Mithali 26 >