< Hesabu 30 >

1 Musa aliwambia viongizi wote wa makabila ya watu wa Israeli. “Hiki ndicho ambacho BWANA ameamuru. 2 Mtu yeyote atakayefanya nadhiri kwa BWANA, au kuapa kwa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asivunje neno lake. Atafanya sawa na ahadi yake imtokayo kinywani mwake. 3 Na kama binti anaishi katika nyumba ya baba yake kwa atafanya nadhiri kwa BWANA na kuifunga nafsi yake kwa kiapo, 4 na kama baba yake atasikia hiyo nadhirina ahadi ambayo ametumia kuifunga nafsi yake, naye asiseme kitu kumzuia, ndipo nadhiri zake zitakuwa na nguvu. Kila ahadi ambayo ameitumia kuifunga nafsi yake itabaki kuwa na nguvu. 5 Lakini kama baba yake atasikia nadhairi yake na ahadi zake, na kama hatasema chochote kwake, ndipo nadhiri zake zote na ahadi alizofanya zitakapokuwa na nguvu. 6 Hata hivyo, kama baba yake atasikia nadhri zake zote alizofanya na ahadi zake makini ambazo ametumia kufunga nafsi yake, na kama atazitengua ndani ya siku hiyo, ndipo hizo nadhiri hazitakuwa na nguvu. BWANA atamsamehe kwa kuwa baba yake amemzuia. 7 Kama ataolewa angali katika hivyo viapo, au kama atafanya ahadi za bila kufikiri ambazo atajifunga nazo, hivyo vifungo vitakuwa na nguvu. 8 Lakini kama mume wake atamzuia siku hiyo hiyo ambayo atamskia akiapa, basi atabatailisha hicho kiapo alichokifanya, maneno yake ya midomo yaka ya bila kufikiri ambayo kwayo amefunga nafsi yake. BWANA atamfungua. 9 Lakini kwa mjane au kwa mwanamke aliyetalikiwa, kila kitu amabacho atakisema kufunga nafsi yake lazima kitabaki na nguvu kinyume na yeye. 10 Na kama mwanamke atafanya kiapo katika nyumba ya mume wake au akijifunga mwenyewe kwa kufanaya kiapo, 11 na mume wake akakisikia hicho kiapo na hakusema chochote kwake na hakumpinga, basi viapo vyake vitasimama na vifungo alivyovifanaya vitabaki na nguvu. 12 Lakini kama mume wake atamzuilia katika siku hiyo ambayo atavisikia, basi chochote ambacho kitatoka katika kinywa chake kuhusu viapo vyake au ahadi zake havitabaki kuwa na nguvu. Mume wake atkuwa amevibatilisha. BWANA atamfungua. 13 Kila kiapo ambacho mwanamke anakifanya ambacho kinamfunga ili kujikana kianaweza kuthibitika au kubatilishwa na mume wake. 14 Lakini kama hatasema chochote kwake siku baada ya siku, basi atathibitisha nadhiri zake na ahadi zake zinazomfunga ambazo amefanya. Atakuwa amezithibitisha kwa sababu hakusema chochote wakati alipozisikia. 15 Na kama mume wake atajariibu kubatilisha kiapo cha mke wake baada ya kuzisikia kwa muda mrefu, basi ataajibika kwa dhambi zake.” 16 Hizi ndizo amri ambazo Mungu alimwamuru Musa kuzitangaza - amri ambazo ziko kati ya mume na mke wake na kati ya baba na binti yake wakati akiwa katika ujana wake katika familia ya baba yake.

< Hesabu 30 >