< Hesabu 24 >

1 Balaamu alipooa kuwa ilimpendeza BWANA kubariki Israeli, hakwenda, kama hapo awali, kwa kutumia uganga, badala yake akatazama jangwani. 2 Akayainua macho yake na kumwona Isreli akiwa kwenye kambi, kila mmoja kwa kabila yake, na Roho wa Mungu akamjia. 3 Akapokea huu unabii na kusema, “Balaamu mwana wa Beori anataka kusema, yeye ambaye macho yake yemefunuliwa sana. 4 Huongea na kusikia maneno ya Mungu. Huona maono toka kwa Mwenyezi, ambaye mbele zake humwinamia na macho yake yakiwa yamefumbuliwa. 5 Jinsi zilivyo nzuri hema zako, ewe Yakobo, mahali unapoishi, Israeli! 6 Wamesambaa kama bonde, kama bustani zilizo pembezoni mwa mto, Kama miti ya mishubiri iliyopandwa na BWANA, ni kama mfano wa mielezi pembezoni mwa maji. 7 Maji yanatiririka katika ndoo zao, na mbegu zao zimemwagiwa maji vizuri. Mfalme wao atakuwa juu ya Agagi, na ufalme wao utaheshimiwa. 8 Mungu anamtoa Misri, na nguvu kama za nyati. Atawameza mataifa wanaopigana nao. Ataivunja mifupa yao katika vipande vipande. atawapiga kwa mishale yake. 9 Ananyatia kama simba mume, na kamaa simba jike. Ni nani atakayejaribu kumsumbua? Kila mmoja anayembariki na abarikiwe; na kila mmoja anayemlaani na alaaniwe.” 10 Hasira za Balaki zikawaka dhidi ya Balaamu naye akaipiga mikono yake kwa pamoja. Balaki akamwambia Balaamu, “Nilkuita ili uwalaani maadui zangu, Lakini tazama, umewabariki mara tatu. 11 Kwa hiyo ondoka uende nyumbani uniache sasa hivi. Nilisema ningekupa zawadi kubwa sana, lakini BWANA amekuzuilia kupata zawadi.” 12 Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, “Niliwaambia wale wajumbe ulionitumia, 13 'Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitafanya zaidi ya maneno ya BWANA kwa lolote zuri au baya, au kwa chochote ambacho ningetaka kufanya. Ninaweza kusema kile tu ambacho BWANA ananiambia kusema,' Je, sikuwaambia haya? 14 Kwa hiyo sasa, tazama, nitarudi kwa watu wangu. Lakini kwanza nikuonye kile ambacho hawa watu watawafanyia watu wako katika siku zijazo.” 15 Balaamu alianza unabii huu. Akisema, “Balaamu mwana wa Beori anasema, Mtu yule aliyefumbuliwa macho yake. 16 Huu ni unabii wa mtu alisikiaye neno la Mungu, aliye na maarifa toka kwake Yeye aliye juu, aliye na maono kutoka kwa Mwenyezi, Yeye ambaye humpigia magoti macho yakiwa yamefumbuliwa. 17 Ninamwona, lakini hayuko hapa sasa. Ninamtazama, lakini siyo karibu. Nyota itatokea katika Yakobo, na fimbp ya enzi itatokea katika Israeli. Naye atawapigapiga viongozi wa Moabu na kuwaharibu wa uzao wa Sethi 18 Ndipo Edomu atakapokuwa miliki ya Israeli, na Seiri pia itakuwa milki yao, maadui wa Israeli, ambao Israeli atawashinda kwa nguvu zake. 19 Kutoka kwa Yakobo atatoka mfalme ambaye utawala wake naye atawaangamiza waliosalia katika mji.” 20 Kisha Balaamu akamtazama Amaleki na akaanza kutoa unabii wake. Alisema, “Amaleki alikuwa mkuu katika mataifa, lakini mwisho wake utakuwa uharibifu.” 21 Kisha Balaamu akawatazama Wakeni na akaanza kutoa unabii wake. Akasema, “Mahali unapoishi pana usalama, na viiota vyake viko kwenye miamba. 22 Lakini pamoja na hayo, Kaini ataharibiwa na Ashuru atakapowachukua mateka.” 23 Kisha Balaamu akanza unabii wake wa mwisho. Akasema, “Ole wake atakayesalia Mungu atakapoyafanya haya? 24 Merikebu zitakuja toka pwani ya Kittimu; Zitaivamia Ashuru na kuiharibu Eberi, lakini wao pia wataishia kwenye uharibifu.” 25 Kisha Balaamu akainuka na kuondoka. Akarudi nyumbani kwake, na Balaki naye akaondoka.

< Hesabu 24 >