< Hesabu 18 >

1 BWANA akamwambia Haruni, “Wewe, wana wako, na uzao wa baba yako watawajibika kwa dhambi zote zilizotendwa mahali patakatifu. Lakini wewe na wana wako pekee mtawajibika kwa uovu uliofanywa na yeyote mahali patakatifu. 2 Na ndugu zako nao wa kabila ya Lawi, kabila la ukoo wako, utawaleta pamoja na wewe ili kwamba waweze kuungana na wewe ili wakusaidie wakati wewe na wanao mnapokuwa mnatumikia mbele ya hema ya amri ya agano. 3 Watakutumikia wewe na hema yote. Hata hivyo, wasisogee karibu na chochote ndani ya mahali patakatifu au kitu chochote kilichounganishwa na madhabahu, vinginevyo wewe na wao mtakufa. 4 Wataungana na wewe na kuitunza hema ya kukutania, kwa kazi zote zinazohusiana na hema. Mtu mgeni asikusogelee. 5 Wewe utaajibika kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya madhabahu ili kwamba hasira yangu isiwajilie watu wa Israeli tena. 6 Tazama, Mmi mwenyewe nimewachagua ndugu zako wa kabila ya Walawi kutoka mioingoni mwa uzao wa Israeli. Wao ni zawadi kwako. walitolewa kwangu ili waifanye kazi inayohusiana na hema ya kukutania. 7 Lakini ni wewe pekee yako na wanao ndio mnaoruhusiwa kufanya kazi ya ukuhani kuhusiana na kila kitu kilichounganishwa na madhabahu na kitu chochote ndani ya lile pazia. Wewe mwenyewe lazima ukamilishe majukumu hayo. Mimi ninakupa ukuhani kama zawadi. Mgeni yeyote anayekaribia atauawa.” 8 Kisha BWANA akamwambia Haruni, “Tazama, Nimekupa majukumu ya kusimamia sadaka za kuinuliwa kwangu, na sadaka zengine takatifu ambazo wana wa Israeli wanatoa kwangu. Nimekupa sadaka hizi wewe na wana wako kuwa haki yako milele. 9 Hivi ni vitu vitakatifu sana, amabavyo visiteketezwe kwa moto: kutoka kwenye sadaka zao-kila sadaka ya unga, kila sadaka ya dhambi, na kila sadaka ya hatia- ni vitu vitakatifu sana kwa ajili yako na wana wako. 10 Sadaka hizi ni takatifu sana; kila mume lazima aile, kwa kuwa ni vitakatifu kwako. 11 Hizi ni sadaka ambazo zitakuwa zako: Sadaka zao, sadaka zote za kuinuliwa za wana wa Israeli. Nimekupa wewe, wana wako na binti zako kuwa gawio lako la milele. Kila mmoja ambaye ni msafi katika familia yako anaweza kula sadaka zozote katika hizi. 12 Mafuta yote mazuri, ile divai nzuri yote mpya na unga, malimbuko ambyo watu hutoa kwangu- vitu hivi vyote nimekupa wewe. 13 Mavuno ya kwanza yaliyoiva yaliyo katika ardhi yao ambayo wanaleta kwangu, yatakuwa yako. Kila mtu aliye msafi kwenye famila yako anaweza kula vitu hivi. 14 Kila kitu kilichotolewa wakfu katika Israeli kitakuwa chako. 15 Kila kitu kinachofungua tumbo, kila limbuko ambalo watu hutoa kwa BWANA, vyote vya watu na wanyama, vitakuwa vyako. Hata hivyo, watu lazima wawakomboe wazaliwa wa kwanza wa kiume, na watawakomboa wazaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi. 16 Wale ambao wanahitaji kukombolewa na watu watakombolewa wakiwa na umri wa mwezi mmoja. Ndipo watu watawakomboa kwa bei ya shekeli tano, kwa kiwango cha shekeli za mahali patakatifu, ambacho ni sawa na gera ishirini. 17 Lakini mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe, au mzaliwa wa kwana wa kondoo, au mzaliwa wa kwanza wa mbuzi-msiwakomboe hawa wanyama, wametengwa kwa ajili yangu. Utanyunyizia damu yake madhabahuni na kuteketeza mafuta yao kama sadaka ya moto, ambayo ni harufu nzuri ya kumpendeza BWANA. 18 Nyama yao itakuwa yako. Kama kidali cha kuinuliwa na paja la kulia, nyama yao itakuwa yako. 19 Sadaka yote takatifu ambayo watu wa Israeli wanaitoa kwa BWANA, nimekupa wewe, na wana wako na binti zako walio pamoja nawe. Kama gawio la kudumu. Hili ni agano la milele la chumvi, agano linalofunga milele, mbele za BWANA kwako wewe na uzao wako walio pamoja na wewe.” 20 BWANA akasema na Haruni. “hautakuwa na urithi katika ardhi ya watu, wala hautakuwa na gawio miongoni mwa watu. Mimi ndimi gawiio lenu na urithi wenu miongoni mwa watu wa Israeli. 21 Tazama, Nimewapatia uzao wa Lawi, zaka zote za Israeli kuwa urithi wao kwa sababu ya huduma wanayotoa katika hema ya kukutania. 22 Kuanzi a sasa, watu wa Israeli wasisogee karibu na hema ya kukutania, vinginevyo wataajibika kwa dhambi hii na kufa. 23 Walawi wafanya kazi inayohusiana na hema ya kukutania. Wataajibika kwa dhambi inyohusiana na hema. Hii itakuwa sheri ya kudumu kwa watu wote wa uzao wako. Na miongoni mwa watu wa Israeli hawa hawatakuwa na urithi. 24 Kwa kuwa zaka za wana wa Israeli, wanazotoa kama mchango kwangu -ndivyo hivyo ambavyo nimewapa Walawi kuwa urithi wao. Hiyo ndiyo sababu ya kuwaambia, Kuwa hawatakuwa na urithi kati ya watu wa Israeli. 25 BWANA akanena na Musa, akamwambia, 26 “Inakupasa ukaseme na Walawi uwaambie, 'Mnapopokea zaka toka kwa watu ambayo BWANA amewapa kutoka kwao kuwa urithi, ndipo na nyie mtakapotoa sehemu ya kumi ya zaka hizo. 27 Zaka yenu itahesabika kama moja ya mapato ya sakafu ya kupuria nafaka ya mazao yenu au mazao ya vinu vya kukamulia zabibu. 28 Kwa hiyo na ninyi lazima mtoe mchango wenu kwa BWANA kutokana na zaka mnazopata kutoka kwa watu wa Israeli. Kutokana na hizo mtatoa matoleo yenu kwa Haruni yule kuhani. 29 Kwa kila sadaka mnayopata, mtatoa matoleo yenu kwa BWANA. Mtafanya hivi kutokana na vitu vizuri na vitakatifu sana ambavyo mmepewa. 30 Kwa hiyo utawaambia, 'Mnapotoa hayo matoleo mazuri, ndipo itahesabika kwa Walawi kuwa ni mazao yao kutoka kwenye sakafu za kupuria na vinu vyao vya kukamulia. 31 Ndipo matakapokula nafaka zote zinazobaki mahali popote, ninyi na famailia zenu kwa sababu ndiyo malipo yenu ya kazi y a kwenye hema ya kukutania. 32 Hamtakuwa na hatia yeyote kwa kuvila na kuvinywa, kama mtatoa kwa BWANA matoleo yenu mazuri mliyopokea. Lakini msizinajisi sadaka takatifu za wana wa Israeli, vinginevyo mtakufa.,”

< Hesabu 18 >