< Mika 2 >

1 Ole wao wale wanao wanaokusudia mabaya, kwa wale wanaokusudia kwenye vitanda vyao kufanya maovu. Katika asubuhi wanayafanya kwa sababu wana nguvu. 2 Wanatamani mashamba na kuyapunguza; wanazitamani nyumba na kuzichukua. Wanadhulumu mtu na nyumba yake, mtu na urithi wake. 3 Kwa hiyo Yahwe asema hivi, “Tazama, nakaribia kuleta janga dhidi ya huu ukoo, ambalo hamtazitoa shingo zenu. Hamtatembea kwa kiburi, kwa kuwa itakuwa wakati wa uovu. 4 Katika siku hiyo maadui zako wataimba wimbo kuhusu wewe, na kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni. Wataimba, 'Sisi Waisraeli tumeangamizwa kabisa; Yahwe hubadilisha eneo la watu wangu. Je ataliondoaje kutoka kwangu? Huwagawia mshamba yetu kusaliti.”' 5 Kwa hiyo, ninyi watu matajiri hamtakuwa uzao kugawanya eneo kwa kupiga kura katika mkutano wa Yahwe. 6 “Msitabiri,” wanasema. “Hawatayatabiri haya mambo; lawama hazitakuja.” 7 Je litasemwa kweli, nyumba ya Yakobo, “je Roho ya Yahwe? Je haya ni matendo yake kweli?” Maneno yangu hayafai kwa kila mmoja atembeaye kwa unyoofu? 8 Hivi karibuni watu wangu wameinuka kama adui. Mmelivua joho, nguo, kutoka wale wapitao wasioshutumiwa, kama maaskari kurudi kutoka kwenye vita kwa kile wakifikiriacho ni salama. 9 Mnawaendesha wanawake wangu kwa watu wangu kutoka kwenye nyumba nzuri; mnachukua baraka kutoka kwa watoto wao wadogo daima. 10 Inukeni na muondoke, kwa kuwa hii sio sehemu ambayo mnaweza kuishi, kwa sababu ya unajisi wake; imeangamizwa kwa maangamizo kabisa. 11 Kama mtu akija kwenu katika roho ya uongo na kudanganya na kusema, “Nitatabiri kwenu kuhusu mvinyo na kilevi kikali,” angeweza kufikiriwa kuwa nabii kwa ajili ya hawa watu. 12 Nitawaleta pamoja wote hakika, Yakobo. Hakika nitawakusanya mabaki ya Israeli. Nitawaleta pamoja kama kondoo katika zizi, kama kundi la wanyama katika malisho. Kutakuwa na kelele kwasababu ya wingi wa watu. 13 Mtu avunjaye hufungua njia zao kwa ajili yao kwenda mbele yao. Wamebomoa kupitia lango na kutoka nje; mfalme wao atapita mbele yao. Yahwe atakuwa mbele yao.

< Mika 2 >